Mashindano ya TotalEnergies CAF Confederation Cup yamerudi kwa kishindo, na timu kubwa za Afrika hazijachelewa kuonyesha makali yao! ⚽🌍
🇹🇿 AZAM FC 2-1 NAIROBI UNITED
Uwanja ulilipuka kwa burudani na drama! Nairobi United walitangulia mapema dakika ya 13 kupitia Dancan Omala, lakini Azam wakajibu haraka dakika ya 17 kupitia Jephté Kitambala.
Dakika ya 78 ikawa ya maamuzi—baada ya mpira wa Himid Mao kugonga mwamba, ukajikuta ukimgonga kipa Ernest Mohammed na kuingia wavuni! 😱 Own goal ya maumivu!
Azam wakasimama imara hadi filimbi ya mwisho na kuendelea kuota ndoto ya robo fainali! 💪🔵
🇿🇦 ZESCO UNITED 0-1 KAIZER CHIEFS
Ndola paligeuka uwanja wa ukimya! Pule Mmodi aliifungia Chiefs bao la mapema kabisa dakika ya 2, na hilo likatosha kuwapa ushindi wa ugenini.
Zesco walishambulia kwa nguvu kipindi chote, lakini kipa Brandon Petersen alikuwa ukuta usiovunjika! 🧤🔥
📌 CAF Confederation Cup inaendelea kuwa moto — nani atasalia, nani ataondoka?
Maoni yako ni yapi? 👇⚽

0 maoni:
Chapisha Maoni